Tuesday, April 17, 2018

MPANGO KAZI MPYA WA CASFETA MKOA WA IRINGA KWA MWAKA 2018.





THE CHRIST’S AMBASSADORS STUDENTS FELLOWSHIP TANZANIA









CASFETA
MKOA WA IRINGA

WAFILIPI 4:13
“NAYAWEZA MAMBO YOTE KATIKA YEYE ANITIAYE NGUVU”.




MPANGO   MKAKATI
2018-2019





‘’MWAKA WA MABADILIKO’’






                                                           


UTANGULIZI
Mpango Mkakati ni nini?
Mpango mkakati ni mfumo wa kimaandishi unaoonyesha kazi zinazotakiwa kufanywa na hatua mbalimbali za kufikia malengo yaliyowekwa kwa muda maalum.
kwa sisi CASFETA – MKOA WA IRINGA, Mpango mkakati unaonyesha utekelezaji na utendaji katika kufikia malengo / makusudi ambayo Mungu anataka tuyafikie kwa Mwaka huu.

UMUHIMU WA MPANGO MKAKATI NI:
·         Kwanza ni muhimu kujua ipo faida kubwa sana kutumia mpango mkakati katika utendaji kazi katika mkoa.
·         Faida na umuhimu wa kuwa na mpango mkakati ni.
Ø  Mpango mkakati huwezesha kuratibu kazi zote ili kufikia lengo.
Ø  Mpango mkakati mara nyingi huleta ufanisi wa utekelezaji wa majukumu kuwa    mazuri.
Ø  Mpango mkakati unatoa mwelekeo wa mkoa, katika kuonyesha njia.
Ø  Mpango mkakati unaonyesha shughuli [kazi zitakazo fanywa na mkoa katika kulitimiza kusudi]
Ø  Mpango mkakati unasaidia kutathimini kama malengo ya mkoa yamefikiwa kwa muda uliopangwa.
Ø  Mpango mkakati husaidia katika mgawanyo wa majukumu miongoni mwa wanachama [kila mtu anajua majukumu yake].
Ø  Mpango mkakati unaweka mpango mzuri wa matumizi ya rasilimali.
Ø  Mpango mkakati unatusaidia kujua vipaumbele vya mkoa.






TUNATEKELEZAJE MPANGO MKAKATI.
v  kila mwanachama/kiongozi anatakiwa kuangalia vipaumbele vya mkoa na kuvifanyia kazi-
v  kila mwanachama/kiongozi kushiriki kutekeleza mikakati au hatua zilizowekwa kutekeleza malengo tuliyojiwekea kama mkoa.
v  kila mwanachama/kiongozi kushiriki kikamilifu katika kalenda ya utendaji tuliyojiwekea kama mkoa.
v  kila mwanachama/kiongozi kushiriki kikamilifu katika kalenda ya utendaji tuliyo tulijiwekea kama mkoa.

IMANI / MAADILI YETU CASFETA
  • kuishi maisha matakatifu, kuishi maisha ya unyenyekevu kujua kuwa sisi ni watumwa wa Bwana.
  • kuwa na nia ya kristo.
  • kudumisha nidhamu, kujinyima baadhi ya vitu ili kutimiza mapenzi ya Mungu [uadilifu]
  • kuonyesha uaminifu, kuhakikisha tunatekeleza tuliyoagizwa kutoka kwa wale wanaotuongoza.
  • tukubali kukosolewa na kuonywa tunajua kuwa hakuna aliye bora kuliko mwingine bali tupo hivi tulivyo kwa neema ya Mungu.   

MAONO
  • Kukua kiroho, kihuduma na kuongezeka kiidadi.
  • kujiimarisha kielimu.

DHAMIRA
  • kujenga kizazi imara kiroho na kimwili.





  MALENGO 
1.      KULETA UAMSHO.
§  kutembelea kanda zote. Tukianzia na kanda zifuatazo: - kalenga na ifunda

§  Ufunguzi wa matawi, jambo hili likisimamiwa na viongozi wa Kanda.

§  Mkutano wa Injili, ambao utafanyikia katika kanda ya Manispaa mnamo Mwezi wa Sita (06) ukiongozwa na Wanacasfeta mkoa mzima.

§  Semina ya Mkoa (Upande wa Vyuo) na Sekondari kwa upande wa kanda.
 
§  Kutembelea makanisa mbalimbali ya kipentekoste yaliyopo ndani ya mkoa wetu
   
§  Huduma za jamii, kwa mfano kuwaona Watoto yatima ambapo tukio hili litafanywa na kila kanda.
  
2.   Kukuza Kiwango Cha Elimu Na Ufaulu.] any people.
  • kuandaa semina za kielimu.
  • Kukusanya mtokeo ya member wote.
  • Kuhamasisha usomaji wa wanacasfeta kupitia Associate Casfeta member na kwa upande wa Sekondari kuhamasisha kupitia Wanavyuo.
  • Kufuatilia matokeo ya wanacasfeta hasa sekondari.

3.   Kutengeneza na Kuandaa Viongozi.
  • kuandaa ibada na semina zenye mkazo juu ya uongozi.
  • kuwahamasisha wanacasfeta kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika serikari ya wanafunzi.
  • kugawa majukumu ya kimaongozi kwa wanacasfeta.

4.  Upatikanaji Wa Ofisi Ya Casfeta Mkoa
  • Ada za uanachama

5.   Miradi ya mkoa.
§   Stetionary.
§  T-shirt





KALENDA YA MATUKIO
MWEZI
TAREHE
TUKIO
WAHUSIKA
SIKU
ENEO




April

7 / 04 / 2018

Kikao

Viongozi wa Casfeta (kamati kuu)

J’mosi

Manispaa(Iringa University)
14 / 04 / 2018
kikao
Viongozi wa casfeta
(kamati kuu na Idara, wakurugenzi)

J’mosi
Manispaa

27-28 / 04 / 2018

Ziara kwenye kanda

Viongzoi wa casfeta mkoa

I’jumaa na j’mosi

Ifunda, na kalenga





May
01 / 05 / 2018
Semina ya wanavyuo

Wanacasfeta wanavyuo
J’nne
Manispaa(Iringa University)
2 - 3 / 05 / 2018
Maombi ya mkoa
Wanacasfeta wote
J’nne hadi alhamis
kanda
05 / 05 / 2018
Semina kwa sekondari
Wanacasfeta kwa  sekondari
J’mosi
Kanda husika
13 / 05 / 2018
Church visity
Wanacasfeta wote
J’pili
Mkimbizi(K.L.P.T)
14 - 18 / 05 / 2018
Ushuhudiaji kimkoa
Wanacasfeta wote
J’tatu - Ijumaa
Kanda
28 - 31 / 05 / 2018
Uhamasishaji wa kongamano la June
Viongozi wote
J’tatu-alhamisi
Kanda


June
1 - 2 / 06 / 2018
Maombi ya kufunga saa 24 kwa viongozi wa CASFETA
Viongozi wote
I’jumaa hadi J’mosi
Mkoa
4 - 8 / 06 / 2018
Leaders’ Conference”Kongamano la Viongozi”
Viongozi na wanachama wote Maadhimisho ya miaka 25 ya CASFETA (Silver Jubilee)
Viongozi wote
J’tatu hadi I’jumaa
Tabora
16 / 06 / 2018
Kikao
Viongozi wote
J’mosi
Manispaa

Kalenda nyingine tutaitoa baada ya tarehe 16 / 06 / 2018.



CASFETA TAIFA.
KANDA SABA ZA MAKONGAMANO

S/N
KANDA
MIKOA HUSIKA
KITUO
01
Kanda ya Kaskazini
Manyara, Arusha, Kilimanjaro.
Manyara
02
Kanda ya Kaskazini Mashariki
Tanga, Zanzibar, Pwani, Dar es Salaam.
Dar es Salaam.
03
Kanda ya Kusini
Rukwa, Songea, Mbeya, Njombe
Rukwa
04
Kanda ya Kusini Mashariki
Mtwara, Lindi, Ruvuma
Lindi
05
Kanda ya Magharibi
Katavi, Kigoma, Tabora
Kigoma
06
Kanda ya Ziwa
Mara, Mwanza, Geita, Kagera, Simiyu, Shinyanga.
Geita
07
Kanda ya Kati
Dodoma, Singida, Morogoro, Iringa
Morogoro


Imeandaliwa na Uongozi wa Casfeta Mkoa, na kutolewa na Ofisi ya makatibu.

Kwa Mawasiliano.
Mwenyekiti Mkoa: 0769 777 689, Katibu Mkoa: 0766 635 382 / 0654 623 492



No comments:

Post a Comment