Sunday, September 3, 2017

Je unaijua CASFETA? Ungana na Rev. Julius Mkenda kujua ukweli wote.

UTANGULIZI:
Rev. Julius Mkenda ni mmoja wa waasisi wa CASFETA ilipoanzishwa mwaka 1993 na kwa saa ni Mkurugenzi wa CASFETA mkoa wa Arusha.
Maana na chimbuko la “JENGA CASFETA“:
Jenga ni kuunda ushirika mmoja katika jambo Fulani, CASFETA ni Christian Ambassador Students Fellowship Tanzania, hivyo inaamaanisha kuunda umoja wa wanafunzi wafwasi wa kristo Tanzania.mnamo mwaka 2008 neno la uhamsho la JENGA CASFETA liliundwa chini ya mchungaji Julius Mkenda na Mch.Nkone, Rejea 1Petro 2:1-10.
NENO:
  Waefeso 2:19-22, bora uwe moto au baridi kwasababu ukiwa vuguvugu Mungu atakutapika hvyo inamaana matapishi yoyote hayawezi kurudiwa lakini huwa yanafunikwa.usitake kutapikwa hujachelewa tubu Leo.
  1wakorintho 6:9-11, huwezi kubarikiwa Kama hujaokoka hata Kama unaketi katikati ya watakatifu.Kwasababu lazima utakuwa na mapungufu ambayo yatapelekea jina la mungu litukanwe.”usionekane mfwasi wa shetani kwa jinsi unavyo vaa au  unavyotenda.
HISTORIA YA CASFETA
CASFETA ilianza mnamo mwaka 1993 chini ya mch.Justine Joseph na Mkenda, mnamo mwaka 1993 ulifanyika mkutano wa kwanza wa Casfeta ulifanyika mkoa wa Kilimanjaro wakishirikiana na mkoa wa Arusha,chini ya jopo la wachungaji na viongozi: Mch.Lazaro, Mch.Shayo,Mkenda na mama Minja.Waliokoka wanafunzi wengi na wanafunzi 70 walibatizwa.
Wanafunzi wa sekondari na vyuo wakisikiliza kwa umakini somo la IJUE CASFETA

MIFUMO ILIYOTUMIKA KUANZISHA NA KUSAJILI CASFETA
  Japo kulikuwa na upinzani mkubwa kutoka kwa ukwata na tycs ushuhudiaji ulifanyika bila uwoga na kupelekea wanafunzi wengi kuhama kutoka matawi mengine na kuhamia casfeta.Suala hili lilileta shida sana katika kusajili Casfeta.Mkuu wa shule za secondary Mr. alexander ndeki aliruhusu casfeta idhaminiwe na umoja wowote lasivyo isingeweza kusajiliwa.
      Hivyo basi wakatafuta kanisa la kipentekosti ambalo  lingeweza  kuidhami CASFETA ili kupata usajili na kutambuliwa  kisheria ,kwa wakati huo  kanisa  la TAG (Tanzania Assembles of God)  lilikua tayari na kuchukua jukumu la kuidhamini CASFETA  kwa niaba ya makanisa yote ya kipentekoste Tanzania ili kuwapatia wanafunzi wa kipentekoste chombo ambacho kinaweza kikawalea katika misingi ya kweli ya kipentekoste wawapo mashuleni na vyuoni.
     Mnamo tarehe 8/10/1993 iliandikwa barua ya maombi kwenda wizara ya elimu kuitambulisha casfeta iliyodhaminiwa na TAG Kwa niaba ya makanisa yote ya kipentekosti.Barua hiyo ilisainiwa na mch.Tytus.
     Mwaka 1994 Casfeta ikiwa chini ya mch.Justine na mch.mkenda na katibu mkuu aliye kuwa mch.uswege mwakisyala Ukwata waliandaa azimio la kuzima nguvu za wana casfeta wakishirikiana na maaskofu wakikatoliki.wakishirikiana kuunda statement ya kuondoa kabisa casfeta.
     Baada ya changamoto nyingi walikutana na mjerumani aliye ahidi kuwafadhili nakuwapa sharti moja la kufungua account ya benki tofauti na casfeta kwa dhumuni lakutaka kuwatumia fedha.
SIRI KUBWA
Mnamo mwaka 1994-1995 iliboru safari lodge jina la kikundi hicho cha vjana kiliundwa rasmi, nacho kiliitwa TANZANIA YOUTH MINISTRY (TAYOMI)chini ya katibu mkuu Mr.Willium Dosa.
Maswali yanayo ulizwa kuhusu TAYOMI:
a)      Kwanini Tayomi iseme imeidhamini CASFETA?
b)      Kwanini Tayomi ikataliwe?
c)       Kwanini migogoro itokee kuhusu Tayomi na Casfeta?
Majibu
·         Migogoro imetokana na barua ya kwanza iliyo pelekwa wizara ya elimu kwamba Casfeta imedhaminiwa na TAG na nyaraka hizo hazija wahi kubadilishwa.
·         Pia TAYOMI ilikuwa ni kwaajili ya kuuingiza pesa kutoka kwa wajerumani haikuwa inahangaika sana na masuala ya Imani ila ilikuwa ni NGO.
·         Tayomi ilisaidia hadi watu ambao hawajaokoka na wengine walikuwa hata sio wakristo kabsa, watu hao pia baadhi walikuwa si wanafunzi bali ni vijana wa mtaani.
UONGO NAMBA MOJA
  Katiba iliundwa na watu wawili yaani Justine na Mkenda,lakini ikiwa na sentensi kwamba “Umoja wa wahudumu wa vijana Tanzania ulioundwa na maaskofu wa kipentekosti”
-          NOTE: hawakuwepo maaskofu wakati katiba inaundwa.
-          Mch.justine alitambua wazi taratibu za TAG kuwa haruhusiwi mchungaji yeyote kufungua tawi au kituchochote nje ya kanisa. Hivyo basi kama angehusisha maaskofu angekuwa anatafuta kufukuzwa. Ni dhahiri kwamba TAYOMI haijahusisha wapentekoste.
UONGO NAMBA MBILI
  Ilihusisha wanachama ambao sio dhahiri,katika usajili wa chama lazima wanachama wawe kumi au Zaidi.majina ya wanachama yalikuwa kama yafuatavyo;
-          Joseph Justine,Julius mkenda,Mrs.mkenda,Solomon mungure,Emmanuel Abraham,Ritha charo na wafuatao hawakuhusika na katiba pia hawakuwa na taarifa na jambo hili;Augenia Justine,Francis shetui,Emmanuel akili, na Elisha Elias.
-          Zaidi ya hao walikuwepo waliosaini pia nao ni;Dr.nazareth mwaipopo,willium dosa na emmanueli mnengule(tabibu wa casfeta)
NOTE: Emmanuel akili alienda kushtaki taarifa za kuundwa Kwa tayomi bila kujua wahusika kwamba nayeye alihusishwa bila kujijua.
UONGO NAMBA TATU
  Kufoji ajenda za kikao ambacho hakija wahi kutokea pia na wanachama ambao hawaja wahi kutokea.
-          Kikao kilifanyika acropol hotel (morogoro) chini ya watu wawili tu ambao ni Mch.Joseph Justine na Mch.Mkenda.
-          Walipewa usajili ambao nyuma yake kulikuwa na majina ya wanachama ambao hawakuwepo na hawana taarifa.
UONGO NAMBA NNE
      Urubuni,walidanganya na kuwashawishi wachungaji wakipentekosti na wanafunzi kujiunga na TAYOMI pia kwamba TAYOMI ni maono waliyo pata kwamba wanafunzi wakimaliza casfeta ingekufa kwahiyo ilihitaji kuwa na wahudumu ambao wangeendelea kuipeleka casfeta mbele.
NOTE:katika katiba kulikuwa na sentensi “waanzilishi wa TAYOMI watakuwa viongozi wa kudumu wa chama hicho”
TAG (magomeni) ndipo mahali ambapo nembo ya CASFETA yenye maandishi madogo ya tayomi kwa chini iliundwa.mwisho kabisa neno TAYOMI lilipanda juu na CASFETA ilishushwa chini. Mnamo mwaka 1997 chuo cha ujenzi morogoro kulikuwa na LEADERS CONFERENCE na TAYOMI ilitangazwa rasmi kuwa inaidhamini CASFETA.
Taarifa ziliifikia TAG na Justine mkenda akafukuzwa kanisani akiitwa “muasi”hivyo kuifadhiwa na Tayomi.Mwaka 2005 mch.mkenda akaacha kazi serikalini na kuamua kuingia na kuijenga TAYOMI.
-          Waliwakataza wanafunzi kutii wachungaji wa TAG,na sumu hiyo ilienea kwa kasi ya ajabu
-          Aliunda programs nyingi ambazo zilikuwa zikihamasisha chama au tawi kwa mfano; “JODAE MOVEMENT” yenye maana kwamba Joseph,Daniel,Ester ambao waliweza kutawala hadi ugenini. Rejea mathayo 16:8
UONGO NAMBA TANO
      Hawakuwa na makuhani,ufanyapo usajili unapaswa kukabidhi barua tatu kutoka kwa maaskofu hvyo basi waliandika barua na kuomba wachungaji Fulani wamakanisa husika kwaajili ya kupiga mihuri barua hizo.
NOTE: mnamo mwaka 2007 mch.mkenda alisikia “UPAKO WA USHIRIKA” akafundishwa itifaki ya MUNGU.
-          Tunatembea juu ya misingi ya mitume na manabii, rejeamathayo 16:8, kwa mfano katika mwili wa binadamu mabega  ndio msingi wa mwili.
-          Itifaki ya MUNGU nikama mwili wa binadamu yaani juu kabisa ya utosi hukaa YESU alafu kichwa ni kuhani,mabega ni msingi alafu ndio hufuatiwa na watu wa kawaida.
-          Rejea zaburi 133:1-3
MWISHO

Kwakumalizia, makanisani kuna watu ambao kunawatu ambao Imani zao ni bandia yaani wamejificha katikati ya kondoo kwa mfano;mguu bandia hauwezi kuhisi chochote chapo hutegemewa sana na mwili katika kuleta usawa wakati wa kutembea.
                              
                    Muhimu: Hii si Casfeta T.A.G,  bali ni Casfeta inayo jumuisha wanafunzi kutoka makanisa yenye Imani ya Kipentekoste, na Inadhaminiwa na Kanisa la T.A.G kwaniaba ya makanisa mengine ya pentekoste..
Source: Casfetadodoma.blogspot.com


No comments:

Post a Comment